Tuesday, 24 February 2015

SIMBA YAINGIA KAMBINI KUIWINDA PRISONS




WEKUNDU wa Msimbazi Simba wameanza mazoezi kujiwinda na mechi ya  ligi kuu soka Tanzania bara itayopigwa jumamosi uwanja wa Taifa, Dar es salaam dhidi ya Maafande wa Jeshi la Magereza, Tanzania Prisons.
Simba waliofungwa bao 1-0 na 'Chama la Wana', Stand United katika mechi ya ligi iliyopigwa uwanja wa CCM Kambarage mwishoni mwa wiki iliyopita wameanza mawindo hayo uwanja wa Jeshi wa JKT Mbweni, Dar es salaam.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa kikosi hicho chini ya kocha mkuu, Goran Kopunovic kitaingia kambini kesho katika Hoteli ya Ndege Beach.
Mechi ya jumamosi inatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na matokeo ya timu zote mbili.
Prisons walitoka suluhu (0-0) dhidi ya Azam fc juzi usiku uwanja wa Azam Complex na kabla ya mechi hiyo walifungwa mabao 3-0 dhidi ya Yanga, Uwanja wa Sokoine.
Wajelajela wanaburuza mkia katika msimamo wa ligi kuu wakijikusanyia pointi 12, wakati Simba wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi nne nyuma ya Kagera Sugar wenye pointi 24.
Katika mechi dhidi ya Azam, Prisons walicheza kwa nidhamu ya hali ya juu na kama wataendeleza moto ule, basi Simba lazima wajipange.

SIMBA SPORT CLUB: KIPIGO CHA STAND UNITED KOCHA SIMBA ANENA

SIMBA SPORT CLUB: KIPIGO CHA STAND UNITED KOCHA SIMBA ANENA: Pamoja na kupoteza nafasi nyingi za kufunga, Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema kweli Ligi Kuu Bara ni ngumu. Kopunovic a...

SIMBA UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU TUWE KITU KIMOJA


avevaaSiku zote unapokuwa puppet au kibaraka kwa lugha ya kiswahili mbali na hilo au kuwa mbabe katika uongozi hakutakuwa na tija hata kidogo na hakutakuwa na matokeo mazuri.
Kingine ni hili suala la matabaka katika sehemu ambayo umoja unahitajika ili kujenga kitu cha msingi ambao utasimama bila kuwa na nyufa ni kama tu unapoanza kujenga nyumba yako mtu wangu, usipotengeneza vizuri msingi wa jambo utaishia kuona nyumba inadondoka au nyufa zinaanza kutokea.
Haya ni mambo mawili ambayo Simba imekumbwa nayo kwa wakati huu na chanzo kikubwa ni uongozi uliopo madarakani bila kupepesa macho.
Matabaka yameiandama Simba toka kwa Uongozi wenyewe hadi kwa wachezaji wenyewe wanakuwa na matabaka.
Ninapoongelea wachezaji nabase moja kwa moja kutokana na jinsi value zao na jinsi wanavyokuwa treated bila usawa. Utakuta yule anapata kila kitu na mwingine hapati kiufupi tu lazima wachezaji hawatakuwa na morality nzuri katika kucheza mpira.
Baadhi ya viongozi au Kiongozi kuzuiwa kuingia katika kambi ya timu lazima pande moja itakuja na mtazamo tofauti na kwa situation hiyo hakuna umoja utakaokuwepo.
Simba kama Brand hakuna haja ya kuwa na matabaka au kutotimiza mahitaji kwa wachezaji hakuna la maana ambalo litafanyika watu wangu.
Nawapongeza Yanga kwasasa walio na umoja na wapo kwenye morality nzuri hivi sasa na imekuwa timu ya kuigwa na haya Simba iwe mfano wa kuiga jinsi Yanga wanavyofanya hivi sasa hakuna kabisa matabaka.
Ni halali yako kushare mawazo yako mtu wangu au kama una breaking News kuhusiana na matukio ya kimichezo au maoni au hata ushauri unaolenga kufika sehemu husika, tuma na tutafikisha sehemu husika mawaidha yako kwa njia ya WhatsApp +255688665508
                                                                                                                                                                                http://shaffihdauda.co.tz/simba-umoja-ni-nguvu-utengano-ni-udhaifu/

KIPIGO CHA STAND UNITED KOCHA SIMBA ANENA


Pamoja na kupoteza nafasi nyingi za kufunga, Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema kweli Ligi Kuu Bara ni ngumu.

Kopunovic amekubali hilo baada ya ile mechi waliyolala kwa bao 1-0 mjini Shinyanga dhidi ya wenyeji Stand United.


Ameiambia SALEHJEMBE kwamba kulikuwa na makosa mengi kwa mwamuzi, pia wachezaji wake kutotumia nafasi, lakini akasisitiza, ligi ni ngumu.

"Ukiangalia mechi utaona tulicheza vizuri tu, lakini kuna makosa kadhaa ya sisi kutotumia nafasi na hata mwamuzi hakuwa mzuri kwetu.

"Lakini bado naweza kusema ligi ni ngumu sana na ushindani uko juu. Kupoteza mechi hiyo na Stand, kweli imeniumiza.

"Najua hata wachezaji wameumia lakini ni suala la kuangalia mechi ipi inafuatia na nini cha kufanya," alisema Kopunovic.

                                                   http://salehjembe.blogspot.com/
                                                                             

Saturday, 6 September 2014

PATRICK PHIRI LAZIMA AIFUNGE GOR MAHIA LEO?


PATRICK-PHIRI-Simba-coach
Kocha mkuu wa Simba sc, Mzambia, Patrick Phiri 
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
KARIBIA mwezi mmoja sasa tangu klabu ya Simba imfungashie virago aliyekuwa kocha mkuu, Mcroatia Zdravko Logarusic.
Tukio hilo lilijiri muda mfupi baada ya Simba kubamizwa mabao 3-0  katika mechi maalumu ya Tamasha la Simba ‘Simba Day’ (Agosti 9 mwaka huu) iliyopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam dhidi ya Zesco United ya Zambia.
Loga katika mechi hiyo alifanya mabadiliko ya wachezaji takribani 8 kwa lengo la kuwajaribu, wakiwemo wale waliokuja kufanya majaribio kutoka Botswana, Kenya na Gambia.
Hata hivyo mabadiliko hayo hayakuinusuruu Simba na kipigo hicho kilichozua mengi hasa baada ya  Loga kuwatamkia maneno mabaya baadhi ya wachezaji wakongwe kama vile Amri Kiemba na Shaaban Kisiga ‘Malone’.
Loga aliyekuwa ametoka kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuinoa Simba alivunjiwa mkataba huo na uongozi wa Simba na hatimaye kuajiriwa kwa Mzambia Patrick Phiri.
Kurudi kwa Phiri kulileta faraja kubwa kwa wachezaji wengi wa Simba waliokuwa wanampinga Loga kutokana na ukali uliozidi kipimo.
Phiri ni kocha anayeifahamu Simba vizuri kwasababu hii ni mara ya tatu kuiongoza, na ana rekodi ya kuipa ubingwa bila kufungwa mwaka 2009.
Ujio wa Mzambia huyo umerudisha morali kwa wachezaji wa Simba waliokuwepo kikosini kabla ya dirisha la usajili na wale waliosajiliwa majira ya kiangazi.
Kwa bahati nzuri kocha huyo anaonekana kupendwa na wapenzi wengi wa Simba wakiwemo viongozi wa ngazi ya juu kwasababu historia inamlinda kwa kiasi kikubwa.
Phiri aliweka kambi kisiwani Unguja na huko ndiko alitumia muda mwingi kuandaa kikosi chake kwa ajili ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Akiwa huko kocha huyu atakayekuwa mpinzani namba moja kwa Marcio Maximo wa Yanga amekuwa akifanyia kazi mambo matatu makubwa katika kikosi cha Simba.
Moja; amekuwa akiwafundisha wachezaji wake namna ya kumiliki mpira kwa asilimia kubwa uwanjani. Lengo la Phiri ni kuifanya Simba icheze zaidi uwanjani ikiwa na mpira ili kuwafanya wapinzani wachanganyikiwe.
Kumiliki mpira kwa kiwango cha juu husaidia zaidi kuwapa presha wachezaji pinzani na kufungua mlango wa kupanga mashambulizi.
Mshambuliaji wa Simba sc, Mkenya Raphael Kiongera (kushoto) akimtoka beki wa Zesco United katika mechi ya Tamasha la Simba Day, Agosti 9 mwaka huu. Msimbazi walilala 3-0 uwanja wa Taifa.
Pili; kocha huyu amekuwa akihangaika kuwafundisha wachezaji wake namna ya upigaji wa pasi sahihi. Lengo ni kufuta pasi zisizokuwa na macho kwa wachezaji wa Simba, Utamaduni wa Simba unaofahamika kwa muda mrefu ni kupiga pasi fupifupi na haraka.
Phiri analifahamu hilo na ndio maana anawajenga wachezaji wake katika msingi huo.
Tatu; Phiri amekuwa akihangaika kuwafundisha wachezaji wake namna ya kupanga mashambulizi ya kasi. Kwa muda mrefu amekuwa akihangaika na safu ya ushambuliaji na kiungo ili ziwe na ushirikiano mzuri wa kupanga mashambulizi ya uhakika.
Pia Phiri amefanya kazi ya kuwaweka pamoja wachezaji baada ya presha ya Loga. Lengo ni kurudisha morali kwa wanandinga hao.
Kama ulibahatika kuiangalia Simba ikicheza Zanzibar akicheza mechi za kirafiki au mazoezi ya Simba kuna kitu kipya kimeongezeka.
Amiss Tambwe (kulia) hayupo leo
Wachezaji wanaonekana kuonana na kucheza kitimu zaidi. Hii ni kwasababu ya kocha Phiri ambaye amewaweka pamoja tena.
Leo hii Simba sc inacheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Hii ni mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki kwa Patrick Phiri tangu arejea Msimbazi. Kitakuwa kipimo kizuri kwake.
Pia mashabiki wa Simba wanaoishi Dar es salaam wataiona timu yao ikicheza uwanja wa Taifa chini ya Phiri, lakini kwa bahati mbaya baadhi ya wachezaji muhimu watakosekana katika kikosi  hicho kutokana na majukumu ya timu ya Taifa.
Joram Mgeveke, Haroun Chanongo, Ramadhan Singano ‘Messi’, Amri Kiemba, hawataonekana leo kwasababu wapo na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi kesho mjini Bujumbura.
Pia Amis Tambwe, Piere Kwizera wapo na timu ya taifa ya Burundi, hivyo watakosekana.
Hata hivyo wachezaji kama Masoud Cholo, Miraji Adam, Hussein Sharrif, Ivo Mapunda, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Uhuru Seleman, Shaaban Kisiga, Said Ndemla, Abdallah Seseme, Abdi Banda, Emmanuel Okwi na wengine ambao sijawataja wataweza kuiwakilisha Simba.
Kimpira, kikosi cha Phiri kitaathirika kwa kiwango fulani kwa kukosa wachezaji muhimu, lakini sio sababu ya kufanya vibaya.
Rais wa Simba sc, Evans Aveva (wa kwanza kushoto) alishuhudia Simba ikichapwa 3-0 na Zesco Tamasha la Simba Day. Kulia ni aliyekuwa kocha wa klabu hiyo, Zdravko Logarusic
Simba ina wachezaji wengi wanaofanya mazoezi na kwa muda aliokaa Simba tangu aanze kazi, Phiri anajua ni nani anaweza kucheza kikosi cha kwanza na mbadala wake ni nani.
Katika mechi za kirafiki Zanzibar, Phiri alikuwa anachezesha vikosi viwili kwa lengo la kupata timu ya kwanza na wachezaji mbadala wa kikosi cha kwanza.
Kwa kuwa bado hajaamua timu ya kwanza ni ipi, kila mchezaji anajituma kutafuta nafasi ya kuonwa. Kwa mazingira hayo kila anayepangwa anapigana kumshawishi Phiri.
Leo hii naitegemea Simba mpya inayocheza pasi za uhakika, kasi ya kutosha, umiliki wa mpira na mashambulizi ya nguvu. Nasema hivi kwasababu Phiri amekuwa akiifundisha timu yake katika aina ya mpira wa hivi.
Lakini siwapi Simba asilimia zote za kushinda mechi ya leo kutokana na aina ya mpinzani wake, ila inaweza kushinda.
Gor Mahia imekaa pamoja kwa muda mrefu na ilishiriki michuano ya kombe la Kagame iliyomalizika mwezi uliopita mjini Kigali, Rwanda.
Japokuwa ilitolewa hatua ya makundi, lakini ilionesha kiwango cha juu na ina wachezaji wazuri wanaoweza kuipa changamoto nzuri Simba.
Kutokana na ubora wa Gor Mahia, nadhani hesabu za Phiri zinatakiwa kukaa sawa zaidi ili kuipa ushindi timu yake.
Phiri akiwa kazini
Hii ni mechi ya kirafiki tu, lakini ina maana kubwa kwa Phiri ili kuwaaminisha mashabiki wa klabu hiyo, ikizingatiwa upande wa pili wamekuwa wakifanya vizuri na katikati ya wiki waliifunga Thika United bao 1-0 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Cha msingi ni kwamba, mashabiki wa Simba lazima watambue kuwa Gor Mahia ni wazuri na si rahisi kuwafunga.
Kama itatokea timu ikacheza tofauti na matarajio yao, watakiwa kuwa na uvumilivu kwasababu ndio kwanza timu inaandaliwa.
Katika mechi za majaribio, makocha wanaangalia vitu vingi. Wachezaji wanajaribiwa kwa nafasi tofauti.Kama ukiona Fulani kapangwa namba tofauti, ujue kuna kitu kocha anakitafuta.
Wanasimba wasiende uwanjani kwa tambo na kuwaangali Yanga wamefanya nini. Phiri na Maximo ni makocha wawili tofauti na aina ya wachezaji wao ni tofauti.
Kama Yanga imeifunga Thika United ya Kenya, sio lazima Simba kuifunga Gor Mahia ya Kenya. Ni timu mbili tofauti.
Phiri ni kocha mzuri na rekodi yake haina wasiwasi kwa Simba, lakini kwa muda huu bado yuko kipindi cha mpito akitafuta timu ya ushindani.
Anaweza kuwatumia wachezaji wengi leo hii kwasababu ni mechi nzuri ya kimataifa ya kirafiki. Lengo lake ni kuona namna wanasoka wake walivyomuelewe.
Nina imani kubwa na Phiri. Ni aina ya makocha ninaodhani wanaweza kulisaidia soka la Tanzania, lakini naamini Wanasimba watampa muda Mzambia huyu.
Rekodi ya nyuma isiwafanye wavimbe vichwa, mpira umebadilika na kutoka 2009 akichukua ubingwa bila kufungwa mpaka sasa kuna mambo mengi yametokea katika mpira wa Tanzania.
Kuna Azam fc, Mbeya City FC, Kagera Sugar, Ruvu Shooting na timu nyinginezo. Upinzani umekuwa mkubwa, hivyo Phiri lazima atahitaji kushindana zaidi.
Kwa mazingira ya sasa, Phiri sio lazima aweke rekodi kama za nyuma na ndio maana hata Jose Mourinho aliyetamba na Chelsea miaka ya 2006, aliporudi msimu uliopita alimaliza bila kikombe.
Sitegemei kuona mashabiki wanaizomea timu kwa namna yoyote ile, kocha anahitaji muda pamoja na wachezaji wake.
Vijana wamekuwa wakifanya mazoezi magumu na mepesi, hata miila yao bado haijawa tayari sana kwa kutandaza soka. Tusitegemee makubwa kutoka kwao katika mchezo wa leo.
Kila la kheri Simba sc katika mchezo wa leo dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
                                                                                                              http://shaffihdauda.com/?p=5872

Wednesday, 27 August 2014

CHANONGO, MAGURI WACHEKA NA NYAVU SIMBA IKIITWANGA MAFUNZO 2-0


Simba imeendeleza wimbi la ushindi kwa kuichapa Mafunzo kwa mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini haoa.
Mabao ya Simba yote mawili yalipatikana katika kipindi cha pili, akianza Elius Maguri katika dakika ya 63.
Shuti lake lilimshinda kipa Khalid Mahadhi, na dakika ya 71, Haruna Chanongo akafunga bao la pili.
Kiungo mkabaji wa Simba, Pierre Kwizera raia wa Burundi alipata balaa baada ya kuumia katika mchezo huo.
Katika mechi iliyopita ya kirafiki, Simba ilishinda kwa mabao 2-1

Sunday, 27 July 2014

SIMBA SC NA AZAM AKADEMI KATIKA PICHA LEO KARUME

SIMBA SC NA AZAM AKADEMI KATIKA PICHA LEO KARUME

Kiungo wa Azam FC, Mudathir Yahya akichuana na kiungo wa Simba SC, Aziz katka mchezo wa Robo Fainali michuano ya Rollingston asubuhi ya leo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Azam FC ilishinda kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 0-0.
Mchezaji wa Azam FC, Sadallah Mohamed kulia akichuana na Aziz wa Simba
Mshambuliaji Jamal Mchaulu 'Balotelli' wa Azam FC akimiliki mpira mbele ya beki wa Simba SC,  Omar Hussein
Mchezaji wa Azam FC, Christopher Mshanga kulia akimtoka mchezaji wa Simba, Omar Hussein
Wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Simba SC, Amisi Tambwe na Shaaban Kisiga walikuwepo Karume kushuhudia wadogo zao
Kiungo wa Azam FC, Malik Mussa kushoto akimtoka beki wa Simba SC, Mbaraka Yussuf
Mchezaji wa Azam FC, Adam Omar akimuacha chini mchezaji wa Simba 
Kocha Mkuu wa Azam FC, Mcameroon Joseph Marius Omog alikuwepo
Kocha Mkuu wa Simba SC, Mcroatia Zradvko Logarusic (katikati) alikuwepo

Friday, 27 June 2014

AMINA POYO APANIA KUFANYA MAKUBWA AKICHAGULIWA SIMBA SC


Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SERA za maendeleo ya klabu ndiyo nyumbani kwake- chochote anachozungumza Amina Hussein Poyo ni juu ya kuleta maafanikio ndani ya klabu ya Simba ya Dar es Salaam.
Mgombea huyo wa nafasi ya Ujumbe upande wa wanawake, miongoni mwa anayotaka kufanya ni kuifufua timu ya wanawake ya Simba SC, maarufu kama Simba Queens ili iweze kuwa tishio za kuzalisha vipaji.
“Itapendeza tunakuwa na timu imara ya Simba Queens, inafanya vizuri kwenye mashindano, tunatoa wachezaji wa timu ya taifa na hata ikibidi kuuza wengine nje, hii itaiongezea umaarufu klabu,”anasema katika mahojiano na BIN ZUBEIRY.
Chagua huyu mama; Amina Poyo ni Simba damu na anatokea familia ya Simba SC tangu enzi za Sunderland

Lakini Simba Queens si mwisho wa fikra za Amina, bali pia amesema atatumia nafasi yake kama Mjumbe wa Kamati ya Utendaji kushawishi harakati za maendeleo ndani ya klabu kwa ujumla.
“Tunataka mafanikio ya uwanjani, kushinda mataji kuanzia ya nyumbani na ya kimataifa. Mimi watu wa Simba wananijua kwa takriban miaka nane iliyopita nimekuwa mstari wa mbele kusaidia na kuhamasisha timu ifanye vizuri.
Ninakwenda hadi kambini ninafanya kazi za timu kwa kujitolea kwa mapenzi yangu, nasafari ndani na nje ya nchi, kwa kweli katika hilo nitafanya zaidi kwa sababu furaha ya kwanza ya wapenzi wa timu ni ushindi wa uwanjani,”anasema.
Amina pia anasema anapenda kuiona Simba SC inakuwa klabu yenye mafanikio ya nje ya uwanja pia kwa kujinufaisha na ukubwa wa jina lake na umaarufu wake kwa kutumia nembo ya klabu kuingiza fedha.
“Hapo namaanisha vitu vingi sana, tunaweza kuuza jezi, fulana, kofia, kanga na vikorokoro vingine vyenye nembo ya Simba SC na tukapata fedha nyingi tu kuisaidia klabu,”anasema.
Amina anasema kwamba atajitolea zaidi kushawishi makampuni mbalimbali yajitokeze kuidhamini timu, akiamini hali ya kiuchumi itakapokuwa nzuri zaidi ndani ya klabu na mambo yatakwenda vizuri.
Kujenga umoja ndani ya klabu na kuondoa makundi na matabata na kuleta maana halisi ya Simba SC “Nguvu Moja” ndiyo ndoto nyingine za Amina Poyo.
Amina anasema kwamba akichaguliwa ndani ya Kamati ya Utendaji ya Simba SC, atahamasisha mradi wa ujenzi wa Uwanja wa klabu hiyo eneo la Bunju, Dar es Salaam ukamilishwe.
Amina Hussein Poyo aliyezaliwa Sikonge mkoani Tabora Julai 11, mwaka 1967 ni mwanachama wa Simba SC tangu mwaka 2008, lakini alianza kuipenda klabu hiyo tangu mdogo kwa sababu anatokea familia ya Simba tangu enzi za Sunderland.
Baba yake marehemu Mikidadi Maruzuku alikuwa mwanachama na mkereketwa maarufu wa Simba SC mjini Mwanza. Amina tayari  ana uzoefu wa kuongoza, hivi sasa akiwa Mwenyekiti wa tawi la Simba la Platinum Saporters. “Chagua Amina Poyo kwa maendeleo ya Simba SC,”anamalizia mwanamama huyo katika mahojiano na BIN ZUBEIRY jana Kigamboni, Dar es Salaam.

Thursday, 26 June 2014

UCHAGUZI SIMBA: Rage aitwa Mahakamani




Mwenyekiti wa Klabu ya Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage. 
Na Vicky Kimaro, Mwananchi

Posted  Alhamisi,Juni26  2014  saa 12:32 PM
KWA UFUPI
Mahakama Kuu imemtaka Rage na Baraza la wadhamini kufika mahakamani hapo leo saa 3:00 asubuhi baada ya wanachama kufungua kesi kupinga uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Juni 29.
Dar es Salaam. Wakati Mahakama Kuu ikimuita mahakamani mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage na baraza lake la wadhamani, wagombea uongozi wa klabu hiyo jana walizindua kampeni zao, huku suala uwanja wake na rasilimali watu likichukua nafasi kubwa.
Mahakama Kuu imemtaka Rage na Baraza la wadhamini kufika mahakamani hapo leo saa 3:00 asubuhi baada ya wanachama kufungua kesi kupinga uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Juni 29.
Wakili Revocatus Kuuli, ambaye anawawakilisha wanachama hao 69 waliofungua kesi na kuomba amri ya kusimamisha uchaguzi huo, alisema leo ndio kesi ya msingi itapangiwa tarehe ya kusikilizwa ikiwa ni pamoja na ombi lao la msingi la kutaka uchaguzi usimame kujulikana.
“Rage na baraza lake la wadhamini wamepelekewa wito wa kuitwa mahakamani kesho (leo) saa 3:00 asubuhi. Sasa kufika au kutofika hiyo ni juu yao. Sisi tunasubiri majibu ya ombi letu ambalo ni kuzuia uchaguzi hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa,” alisema Kuuli.
Hadi jana jioni, Rage alikuwa mjini Dodoma ambako anashiriki kwenye Bunge la Bajeti na alichangia hoja majira ya saa 12:15.
Wanachama 69 wanaowakilishwa na Hassan Abdallah, Josephat Waryoba na Said Ally, walifungua kesi wakitaka izuie kufanyika uchaguzi huo kwa kile walichodai kuwa katiba imekiukwa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba haijaundwa kikatiba.
Pia, wanachama hao wa Simba wanalalamikia kutokuwapo kwa Kamati ya Maadili iliyotakiwa kuundwa kwa ajili ya kusikiliza masuala mengi yahusuyo maadili ambayo hadi sasa hayajatatuliwa.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, katibu mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema:
“Sijui lolote... sina taarifa kama kuna wito ambao umetolewa na mahakama. Sikuwapo ofisini, labda kama taarifa hiyo ilipelekwa ofisini.”
Hata hivyo, wakati mahakama ikitoa wito huo, mgombea wa nafasi ya urais, Evans Aveva alisema atampa muda wa kujitathmini kocha wa timu hiyo, Zradvko Logarusic kabla ya kutoa nafasi zaidi kwa makocha wazawa.
“Nitawapa kipaumbele makocha wazalendo, lakini kwanza sina budi kutoa nafasi kwa Loga. Tutaangalia uwezo wake na matakwa yetu kisha tutaamua,” alisema.
Aveva alisema Simba, ambayo ina miaka 78 tangu kuanzishwa kwake, hailingani na hadhi yake kwa kuwa imeshindwa kujiendesha kiuchumi na kumiliki uwanja. “Kwa sasa Simba ina wanachama 7,000 nitajitaidi ndani ya miaka minne wafikie 50,000 ili kuitoa Simba hapa ilipo.”

NIGERIA YACHAPWA 3-2 NA ARGENTINA, LAKINI YAFUZU HATUA YA 16 KOMBE LA DUNIA



article-2669577-1F1F61DB00000578-837_634x363
Nyota: Lionel Messi (juu) aliifungia mabao mawili Argentina dhidi ya Nigeria.
 
TIMU ya Taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 ya kombe la dunia licha ya kufungwa mabao 3-2 dhidi ya Argentina.
Mshambuliaji hatari wa kikosi cha Alejandro Sabella, Lionel Messi amefunga mabao mawili katika dakika ya 3 na 45  katika ushindi uliowapa Argentina ushindi wa asilimia 100 katika kundi lao la F.
Bao la tatu la Argentina limefungwa na Marcos Rojo katika dakika ya 50.
Mabao mawili ya Nigeria yamefungwa na Ahmed Musa katika dakika ya 4 na 47.
Katika michuano ya mwaka huu, dhahiri, Argentina inamtegemea zaidi Messi katika mechi zake.
Baada ya kufunga mabao hayo, kocha Sabella alimpumzisha nyota huyu wa FC Barcelona kwa ajili ya mikikimikiki ya hatua ya 16.
Pia Sabella alishuhudia mshambuliaji wake, Sergio Kun Aguero akitolewa nje ya uwanja kwa kile kilichoonekana kupata maumivu ya misuli tena.
Main man: Messi (right) put his side into a 1-0 with this strike after just three minutes
Thank you: Messi points to the sky in celebration after his first goal of the game
 Asante mungu: Messi akinyosha vidole kama ishara ya kumshukuru mungu baada ya kufunga .
Hapa chini ni vikosi vya timu zote na viwango vya wachezaji. Alama ni chini ya 10.
Kikosi cha Argentina (4-3-3): Romero 7; Zabaleta 6, Federico Fernandez 5, Garay 5, Rojo 6; Gago 7, Mascherano 6, Di Maria 8; Messi 9 (Alvarez 19 6), Higuain 6 (Biglia 90 6), Aguero 6 (Lavezzi 37 7). 

Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Orion, Campagnaro, Perez, Maxi Rodriguez, Augusto Fernandez, Demichelis, Palacio, Basanta, Andujar.
Wafungaji wa bao: Messi 3, 45′, Rojo 50′
Kocha: A Sabella 6
Kikosi cha Nigeria (4-5-1): Enyeama 7; Ambrose 6, Yobo 6, Oshaniwa 5, Omeruo 6; Odemwingie 6 (Nwofor 80 6), Onazi 6, Mikel 6, Babatunde 7 (Uchebo 66 6), Musa 8; Emenike 7.

Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Ejide, Uzoenyi, Gabriel, Egwuekwe, Odunlami, Oboabona, Azeez, Ameobi, Agbim.
Mchezaji bora wa mechi: Messi
Kocha: S Keshi 7
Kadi ya njano: Omeruo, Oshaniwa

Mfungaji wa mabao: Musa 4′, 47′

Mwamuzi: Nicola Rizzoli
*Viwango vya wachezaji na MATT LAWTON katika uwanja Porto Alegre
Jubilant: Messi (left), Di Maria (centre) and Marcos Rojo celebrate the opening goal
Double: Ahmed Musa (left) grabbed his first World Cup brace to give Nigeria hope
  Ahmed Musa (kushoto) alifunga mabao mawili katika mchezo wa leo.
Happy family: Musa ran towards the bench to enjoy his second goal with his team-mates
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=2537#sthash.vKFQS0Yo.dpuf

EVANS AVEVA ALIVYOZINDUA KAMPENI ZAKE TEMEKE LEO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU SIMBA SC, HANS POPPE NA KABURU NDANI YA NYUMBA

Mgombea Urais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva akizungumza na wanachama wa Temeke katika ukumbi wa Kata ya 14, jioni ya leo wakati wa uzinduzi wa kampeni zake kuelekea uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo Juni 29, mwaka huu mjini Dar es Salaam.
Aveva katikati akizungumza, kulia ni Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Hassan Daalal na kushoto ni mfadhili wa klabu hiyo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe
Wanachama wa Simba SC wakimsikiliza Aveva
Babu huyu akimsikiliza kwa makini Aveva wakati akimwaga sera zake
Akina mama nao hawakubaki nyuma
Aveva akisikiliza maoni, maswali na ushauri wa wanachama wa Temeke
Kutoka kulia Daalal, Aveva na Geoffrey Nyange 'Kaburu' mgombea Umakamu wa Urais
Hans Poppe, Kaburu na Aveva
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Temeke (TEFA), Peter Mhinzi akimuombea kura Aveva kwa wanachama hao
Mikono juu, wanachama wakionyesha ishara watamoa kura Aveva
Aveva akisalimiana na mwanachama mlemavu wa Simba SC baada ya kampeni zake