Friday, 27 June 2014

AMINA POYO APANIA KUFANYA MAKUBWA AKICHAGULIWA SIMBA SC


Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SERA za maendeleo ya klabu ndiyo nyumbani kwake- chochote anachozungumza Amina Hussein Poyo ni juu ya kuleta maafanikio ndani ya klabu ya Simba ya Dar es Salaam.
Mgombea huyo wa nafasi ya Ujumbe upande wa wanawake, miongoni mwa anayotaka kufanya ni kuifufua timu ya wanawake ya Simba SC, maarufu kama Simba Queens ili iweze kuwa tishio za kuzalisha vipaji.
“Itapendeza tunakuwa na timu imara ya Simba Queens, inafanya vizuri kwenye mashindano, tunatoa wachezaji wa timu ya taifa na hata ikibidi kuuza wengine nje, hii itaiongezea umaarufu klabu,”anasema katika mahojiano na BIN ZUBEIRY.
Chagua huyu mama; Amina Poyo ni Simba damu na anatokea familia ya Simba SC tangu enzi za Sunderland

Lakini Simba Queens si mwisho wa fikra za Amina, bali pia amesema atatumia nafasi yake kama Mjumbe wa Kamati ya Utendaji kushawishi harakati za maendeleo ndani ya klabu kwa ujumla.
“Tunataka mafanikio ya uwanjani, kushinda mataji kuanzia ya nyumbani na ya kimataifa. Mimi watu wa Simba wananijua kwa takriban miaka nane iliyopita nimekuwa mstari wa mbele kusaidia na kuhamasisha timu ifanye vizuri.
Ninakwenda hadi kambini ninafanya kazi za timu kwa kujitolea kwa mapenzi yangu, nasafari ndani na nje ya nchi, kwa kweli katika hilo nitafanya zaidi kwa sababu furaha ya kwanza ya wapenzi wa timu ni ushindi wa uwanjani,”anasema.
Amina pia anasema anapenda kuiona Simba SC inakuwa klabu yenye mafanikio ya nje ya uwanja pia kwa kujinufaisha na ukubwa wa jina lake na umaarufu wake kwa kutumia nembo ya klabu kuingiza fedha.
“Hapo namaanisha vitu vingi sana, tunaweza kuuza jezi, fulana, kofia, kanga na vikorokoro vingine vyenye nembo ya Simba SC na tukapata fedha nyingi tu kuisaidia klabu,”anasema.
Amina anasema kwamba atajitolea zaidi kushawishi makampuni mbalimbali yajitokeze kuidhamini timu, akiamini hali ya kiuchumi itakapokuwa nzuri zaidi ndani ya klabu na mambo yatakwenda vizuri.
Kujenga umoja ndani ya klabu na kuondoa makundi na matabata na kuleta maana halisi ya Simba SC “Nguvu Moja” ndiyo ndoto nyingine za Amina Poyo.
Amina anasema kwamba akichaguliwa ndani ya Kamati ya Utendaji ya Simba SC, atahamasisha mradi wa ujenzi wa Uwanja wa klabu hiyo eneo la Bunju, Dar es Salaam ukamilishwe.
Amina Hussein Poyo aliyezaliwa Sikonge mkoani Tabora Julai 11, mwaka 1967 ni mwanachama wa Simba SC tangu mwaka 2008, lakini alianza kuipenda klabu hiyo tangu mdogo kwa sababu anatokea familia ya Simba tangu enzi za Sunderland.
Baba yake marehemu Mikidadi Maruzuku alikuwa mwanachama na mkereketwa maarufu wa Simba SC mjini Mwanza. Amina tayari  ana uzoefu wa kuongoza, hivi sasa akiwa Mwenyekiti wa tawi la Simba la Platinum Saporters. “Chagua Amina Poyo kwa maendeleo ya Simba SC,”anamalizia mwanamama huyo katika mahojiano na BIN ZUBEIRY jana Kigamboni, Dar es Salaam.

Thursday, 26 June 2014

UCHAGUZI SIMBA: Rage aitwa Mahakamani




Mwenyekiti wa Klabu ya Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage. 
Na Vicky Kimaro, Mwananchi

Posted  Alhamisi,Juni26  2014  saa 12:32 PM
KWA UFUPI
Mahakama Kuu imemtaka Rage na Baraza la wadhamini kufika mahakamani hapo leo saa 3:00 asubuhi baada ya wanachama kufungua kesi kupinga uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Juni 29.
Dar es Salaam. Wakati Mahakama Kuu ikimuita mahakamani mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage na baraza lake la wadhamani, wagombea uongozi wa klabu hiyo jana walizindua kampeni zao, huku suala uwanja wake na rasilimali watu likichukua nafasi kubwa.
Mahakama Kuu imemtaka Rage na Baraza la wadhamini kufika mahakamani hapo leo saa 3:00 asubuhi baada ya wanachama kufungua kesi kupinga uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Juni 29.
Wakili Revocatus Kuuli, ambaye anawawakilisha wanachama hao 69 waliofungua kesi na kuomba amri ya kusimamisha uchaguzi huo, alisema leo ndio kesi ya msingi itapangiwa tarehe ya kusikilizwa ikiwa ni pamoja na ombi lao la msingi la kutaka uchaguzi usimame kujulikana.
“Rage na baraza lake la wadhamini wamepelekewa wito wa kuitwa mahakamani kesho (leo) saa 3:00 asubuhi. Sasa kufika au kutofika hiyo ni juu yao. Sisi tunasubiri majibu ya ombi letu ambalo ni kuzuia uchaguzi hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa,” alisema Kuuli.
Hadi jana jioni, Rage alikuwa mjini Dodoma ambako anashiriki kwenye Bunge la Bajeti na alichangia hoja majira ya saa 12:15.
Wanachama 69 wanaowakilishwa na Hassan Abdallah, Josephat Waryoba na Said Ally, walifungua kesi wakitaka izuie kufanyika uchaguzi huo kwa kile walichodai kuwa katiba imekiukwa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba haijaundwa kikatiba.
Pia, wanachama hao wa Simba wanalalamikia kutokuwapo kwa Kamati ya Maadili iliyotakiwa kuundwa kwa ajili ya kusikiliza masuala mengi yahusuyo maadili ambayo hadi sasa hayajatatuliwa.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, katibu mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema:
“Sijui lolote... sina taarifa kama kuna wito ambao umetolewa na mahakama. Sikuwapo ofisini, labda kama taarifa hiyo ilipelekwa ofisini.”
Hata hivyo, wakati mahakama ikitoa wito huo, mgombea wa nafasi ya urais, Evans Aveva alisema atampa muda wa kujitathmini kocha wa timu hiyo, Zradvko Logarusic kabla ya kutoa nafasi zaidi kwa makocha wazawa.
“Nitawapa kipaumbele makocha wazalendo, lakini kwanza sina budi kutoa nafasi kwa Loga. Tutaangalia uwezo wake na matakwa yetu kisha tutaamua,” alisema.
Aveva alisema Simba, ambayo ina miaka 78 tangu kuanzishwa kwake, hailingani na hadhi yake kwa kuwa imeshindwa kujiendesha kiuchumi na kumiliki uwanja. “Kwa sasa Simba ina wanachama 7,000 nitajitaidi ndani ya miaka minne wafikie 50,000 ili kuitoa Simba hapa ilipo.”

NIGERIA YACHAPWA 3-2 NA ARGENTINA, LAKINI YAFUZU HATUA YA 16 KOMBE LA DUNIA



article-2669577-1F1F61DB00000578-837_634x363
Nyota: Lionel Messi (juu) aliifungia mabao mawili Argentina dhidi ya Nigeria.
 
TIMU ya Taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 ya kombe la dunia licha ya kufungwa mabao 3-2 dhidi ya Argentina.
Mshambuliaji hatari wa kikosi cha Alejandro Sabella, Lionel Messi amefunga mabao mawili katika dakika ya 3 na 45  katika ushindi uliowapa Argentina ushindi wa asilimia 100 katika kundi lao la F.
Bao la tatu la Argentina limefungwa na Marcos Rojo katika dakika ya 50.
Mabao mawili ya Nigeria yamefungwa na Ahmed Musa katika dakika ya 4 na 47.
Katika michuano ya mwaka huu, dhahiri, Argentina inamtegemea zaidi Messi katika mechi zake.
Baada ya kufunga mabao hayo, kocha Sabella alimpumzisha nyota huyu wa FC Barcelona kwa ajili ya mikikimikiki ya hatua ya 16.
Pia Sabella alishuhudia mshambuliaji wake, Sergio Kun Aguero akitolewa nje ya uwanja kwa kile kilichoonekana kupata maumivu ya misuli tena.
Main man: Messi (right) put his side into a 1-0 with this strike after just three minutes
Thank you: Messi points to the sky in celebration after his first goal of the game
 Asante mungu: Messi akinyosha vidole kama ishara ya kumshukuru mungu baada ya kufunga .
Hapa chini ni vikosi vya timu zote na viwango vya wachezaji. Alama ni chini ya 10.
Kikosi cha Argentina (4-3-3): Romero 7; Zabaleta 6, Federico Fernandez 5, Garay 5, Rojo 6; Gago 7, Mascherano 6, Di Maria 8; Messi 9 (Alvarez 19 6), Higuain 6 (Biglia 90 6), Aguero 6 (Lavezzi 37 7). 

Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Orion, Campagnaro, Perez, Maxi Rodriguez, Augusto Fernandez, Demichelis, Palacio, Basanta, Andujar.
Wafungaji wa bao: Messi 3, 45′, Rojo 50′
Kocha: A Sabella 6
Kikosi cha Nigeria (4-5-1): Enyeama 7; Ambrose 6, Yobo 6, Oshaniwa 5, Omeruo 6; Odemwingie 6 (Nwofor 80 6), Onazi 6, Mikel 6, Babatunde 7 (Uchebo 66 6), Musa 8; Emenike 7.

Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Ejide, Uzoenyi, Gabriel, Egwuekwe, Odunlami, Oboabona, Azeez, Ameobi, Agbim.
Mchezaji bora wa mechi: Messi
Kocha: S Keshi 7
Kadi ya njano: Omeruo, Oshaniwa

Mfungaji wa mabao: Musa 4′, 47′

Mwamuzi: Nicola Rizzoli
*Viwango vya wachezaji na MATT LAWTON katika uwanja Porto Alegre
Jubilant: Messi (left), Di Maria (centre) and Marcos Rojo celebrate the opening goal
Double: Ahmed Musa (left) grabbed his first World Cup brace to give Nigeria hope
  Ahmed Musa (kushoto) alifunga mabao mawili katika mchezo wa leo.
Happy family: Musa ran towards the bench to enjoy his second goal with his team-mates
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=2537#sthash.vKFQS0Yo.dpuf

EVANS AVEVA ALIVYOZINDUA KAMPENI ZAKE TEMEKE LEO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU SIMBA SC, HANS POPPE NA KABURU NDANI YA NYUMBA

Mgombea Urais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva akizungumza na wanachama wa Temeke katika ukumbi wa Kata ya 14, jioni ya leo wakati wa uzinduzi wa kampeni zake kuelekea uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo Juni 29, mwaka huu mjini Dar es Salaam.
Aveva katikati akizungumza, kulia ni Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Hassan Daalal na kushoto ni mfadhili wa klabu hiyo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe
Wanachama wa Simba SC wakimsikiliza Aveva
Babu huyu akimsikiliza kwa makini Aveva wakati akimwaga sera zake
Akina mama nao hawakubaki nyuma
Aveva akisikiliza maoni, maswali na ushauri wa wanachama wa Temeke
Kutoka kulia Daalal, Aveva na Geoffrey Nyange 'Kaburu' mgombea Umakamu wa Urais
Hans Poppe, Kaburu na Aveva
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Temeke (TEFA), Peter Mhinzi akimuombea kura Aveva kwa wanachama hao
Mikono juu, wanachama wakionyesha ishara watamoa kura Aveva
Aveva akisalimiana na mwanachama mlemavu wa Simba SC baada ya kampeni zake 

Monday, 17 March 2014

KAPOMBE AREJESHWA SIMBA SC, KUANZA TENA KAZI MSIMU UJAO, HANS POPPE AMALIZANA NA WAFARANSA


Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
KIUNGO anayeweza kucheza nafasi za ulinzi pia, Shomary Kapombe atarejea kwenye kikosi cha Simba SC msimu ujao baada ya makubaliano yaliyofikiwa baina ya klabu hiyo na AS Cannes ya Ufaransa.
Habari za ndani kutoka Simba SC ambazo BIN ZUBEIRY imezipata, zinasema kwamba Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amefikia makubaliano mazuri na AS Cannes juu ya Kapombe.
Anarudi nyumbani; Shomary Kapombe atarejea kwenye kikosi cha Simba SC msimu ujao 
“Poppe amezungumza na Cannes na wamekubaliana kulipana fedha ili Kapombe arejee Simba SC,” kimesema chanzo kutoka Simba SC na alipotafutwa Poppe mwenyewe alisema; “Nipo safarini, lakini kwa kifupi Kapombe anarudi Simba SC kwa Mkataba wa miaka mitatu kuanzia msimu ujao,”alisema.    
Poppe amesema kwamba Simba SC imekubali kuilipa Cannes Euro 33,000 ambazo sawa na Sh. Milioni 66 ili kurejeshewa mchezaji wake huyo.
Wakati wa kuimarisha timu; Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amemalizana na Cannes Kapombe arejee Msimbazi 

Kapombe alitolewa bure kwenda AS Cannes katikati ya mwaka jana akiwa bado ana Mkataba na klabu hiyo ya Msimbazi, unaomalizika Aprili mwaka huu.
Baada ya kuwa Ufaransa kwa zaidi ya miezi mitatu, Kapombe alirejea nchini Novemba mwaka jana kwa ruhusa maalum ya kuja kuichezea timu ya taifa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe.  
Baada ya mchezo huo, mchezaji huyo akaamua kubaki moja kwa moja nyumbani akidai halipwi mishahara.
Kapombe mwenyewe amekuwa mgumu kuzungumzia suala hilo, lakini tayari kuna habari kwamba Yanga SC na Azam zinamtaka mchezaji huyo
                                              
                                                                 SOURCE http://bongostaz.blogspot.com/

Tuesday, 4 March 2014

BREAKING NEWS! RIDHIWANI AMWANGUSHA MADEGA KWENYE KURA ZA MAONI HUKO CHALINZE!




Kuelekea uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani lililoachwa wazi baada ya mbunge wake SAID BWANAMDOGO kufariki hivi karibuni Chama cha Mapinduzi kimefanya kura ya maoni ili kumpata mrithi wa Jimbo hilo atakayechuana na wagombea kutoka vyama vingine.



Katika kura hiyo ya maoni wagombea watatu wamejitokeza kuwania nafasi ya ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia chama cha CCM akiwemo mbunge wa zamani wa Jimbo hilo RAMADHAN MANENO, mwenyekiti wa zamani wa Yanga IMANI MADEGA na mdau mkubwa wa soka hapa nchini na mwanachama wa Yanga RIDHIWANI KIKWETE.
Baada ya kura kupigwa RIDHIWANI KIKWETE ndiye amepata Baraka za wanaCCM kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge kwa kumpa kura 758 huku IMANI MADEGA akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 335 na RAMADHAN MANENO akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 206.                                                                                                                                                         source http://www.shaffihdauda.com/