,
Hatimaye wabishi wa Mbeya City wamekubali kipigo cha pili katika Ligi Kuu Bara baada ya kufungwa bao 2-0 na wenyeji Coastal Union.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, mabao yote ya Coastal Union, yamefungwa na Mohammed Miraji.
Tokea kuanza kwa ligi hiyo, City walikuwa wamepoteza mechi moja tu dhidi ya Yanga kwa kufungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Kikosi hicho cha Juma Mwambusi kilifanikiwa kumaliza mzunguko wa kwanza bila ya kufungwa hata mechi moja.
http://salehjembe.blogspot.com/

No comments:
Post a Comment