LOGARUSIC ATAKA SARE YA MBEYA CITY ISIWE GUMZO
Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema sare dhidi ya Mbeya City haiwezi kukifanya kikosi chake kuyumba kwa kuwa wanaamini sare ni sehemu ya mchezo.
Simba imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wake Mbeya City katika mechi iliyopigwa jana kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
“Kweli tumepata sare na tulichotaka ni kushinda, vijana walijitahidi na hakuna sababu ya kukata tamaa,” alisema Logarusic.
“Tutaendelea kupambana hadi mwisho kwa kuwa ligi bado ina nafasi za kuendelea kushinda kama tutajiandaa vema na kuwa makini.
“Kwetu suala la Mbeya City limepiga na sasa tunachoangalia ni mechi inayofuata na hakuna zaidi,” alisema Logarusic.
Rekodi ya Simba katika Ligi Kuu Bara chini ya kocha huyo inaonyesha hivi, ameiongoza katika mechi tano, ameshinda mbili, amepoteza moja na sare mbili.
SOURCE http://salehjembe.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment